Hata
hivyo, wawili hao wamesema wanahisi wito huo unatokana na mkutano wa
hadhara alioitisha Sugu katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini
Mbeya.
Akizungumza
kwa simu leo Jumanne Januari 2,2018 Sugu amesema juzi jioni alipigiwa
simu na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya (RCO) kwamba pamoja na Masonga
wafike jana ofisini kwake kuzungumza lakini alimueleza ilikuwa ni siku
ya sikukuu hivyo itakuwa ngumu kwenda, hivyo walikubaliana wafike leo.
"Walinipigia
simu juzi jioni wakinitaka mimi na Masonga twende makao makuu ya polisi
jana, nikawaambia itakuwa ni sikukuu hivyo tukakubaliana leo asubuhi,
hivyo tupo njiani tunaelekea huko kuitika wito. Sijajua sababu, lakini
nadhani ni uchochezi," amesema Sugu.
Masonga amesema anaamini sababu ya kuitwa kwao inatokana na mkutano wao na wananchi.
Amesema
katika mkutano huo yeye Masonga ndiye aliyemkaribisha Sugu kuzungumza
na wananchi na alifunga mkutano, lakini kabla ya kumkaribisha
alizungumza machache kuhusu mustakabali wa Taifa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga hajapatikana ili kuzungumzia wito huo wa akina Sugu.
0 comments:
Post a Comment