Mbunge
wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ambaye yuko Nairobi
nchini Kenya kwa matibabu, amesema kuwa Bunge la Tanzania halijatoa pesa
yoyote kugharamia matibabu yake, kauli ambayo inatofautiana na Bunge
ambayo ilisema imetuma fedha.
Akizungumza
kwenye mahojiano na moja ya television za hapa nchini, Tundu Lissu
amesema hakuna pesa yoyote iliyotolewa na Bunge wala serikali, kwa ajili
ya matibabu yake huko nchini Kenya.
"Bunge
halijatoa hata senti moja ya matibabu yangu, serikali haijatoa hata
senti moja, familia yangu na ndugu zangu inasema mbunge amelazwa tangu
Septemba 7, Spika wa Bunge hajaenda, Naibu Spika wa Bunge hajaenda,
Katibu wa Bunge hajaenda, Tume ya huduma za Bunge haijaja, haijatoa hata
senti 10 kugharamia matibabu yangu", amesema Tundu Lissu.
Mnamo
Septemba 7, 2017, Mbunge Tundu Lisu alipigwa risasi na watu
wasiojulikana, tukio ambalo limemfanya alazwe hospitali kwa zaidi ya
miezi mitatu mpaka sasa akipatiwa matibabu, na Bunge lilitoa taarifa
kuwa limetuma pesa za matibabu, ambazo hospitali ambayo Tundu Lissu yupo
akitibiwa ilikiri kuzipokea kwenye acount yake.
0 comments:
Post a Comment