Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu amekiri kwamba hatakuja
kusahau tukio la mkazi wa Iringa aliyekwenda hospitali Nairobui
alikolazwa kwa ajili ya kumuombea ili apate kupona baada ya kupigwa
risasi na watu wasiojulikana.
Lissu
ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na chombo kimoja cha habari
nchini, amedai kwamba mama huyo alimgusa sana kwa upendo aliouonyesha
juu yake huku akizingatia kwamba ametokea mbali sana huku akionekana ni
mtu wa hali ya chini.
"Ukiwa
mgonjwa kisha akaja mtu kukutembelea ni faraja sana. Nawashukuru maelfu
ya watanzania na watu wote waliofika Nairobi kunijulia hali. Lakini
sitakaa kuweza kumsahau mama mmoja aliyetoka Iringa kwa ajili ya kuja
kuniombea," Lissu.
Lissu
ameongeza "Aliniambia Mheshimiwa nimetokea Iringa na mpaka nimefika
hapa nimetumia siku tano. Nikamwambia mama asante niombee kisha akapiga
magoti na kuniombea. Alinigusa sana na ukimuangalia mama yule unatambua
kabisa hajatokea mjini na hata hali yake ya uchumi siyo nzuri lakini
ulikuwa ni upendo wa ajabu ambao ulinigusa sana".
Mbunge
Lissu yupo hospital ya Nairobi akipatiwa matibabu baada ya kupigwa
risasi na watu wasiojulika huko mkoani Dodoma wakati akiwa ametokea
kazini (bungeni) Septemba 07, 2017
0 comments:
Post a Comment