Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa
CHADEMA Kanda ya Nyassa, Emmanuel Masonga wamerudishwa rumande hadi
Januari 22, 2018 siku ya Jumatatu ambapo kesi yake itaanza kusomwa
mfululizo.
Mbunge
huyo wa Mbeya mjini na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa wanashikiliwa
na jeshi la polisi wakituhumiwa kutenda kosa la uchochezi katika mkutano
wao wa hadhara ambao ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya ambapo
jeshi la polisi linasema kuwa viongozi hao walizungumza maneno yenye
kuleta chuki kati ya Serikali na wananchi.
Mchana
wa January 16, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Mbeya iliamuru
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu na Katibu wa
CHADEMA Kanda ya Nyassa Emmanuel Masonga wapelekwe rumande mpaka January
19 ambayo ni leo kwa kesi ya uchochezi.
Viongozi hao wamerudishwa rumande tena mpaka siku ya Jumatatu ambapo kesi yao itaanza kusomwa tena
0 comments:
Post a Comment