Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemchukua Makamu wa Rais
wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ anayekabiliwa na kesi ya
utakatishaji fedha wa USD 300,000 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
kwa ajili ya kumuhoji.
Mbali ya Kaburu, mshtakiwa mwingine ni Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva ambaye hakufika mahakamani hapo.
Mwendesha
Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu,
Victoria Nongwa kwamba kesi hiyo haikupangwa leo isipokuwa wamemtoa
Kaburu gerezani kwa kibali ili akahojiwe.
Baada
ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa alimkabidhi Kaburu kwa Wakili Swai huku
akimtaka amrudishe leo kama alivyoomba, ambapo aliahirisha kesi hiyo
hadi tarehe iliyopangwa January 25,2018.
Aveva
na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi,
kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya
kuhamisha fedha ya Machi 15, 2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa
mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.
0 comments:
Post a Comment