Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amempongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, kwa
kuiongoza nchi vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017.
Seif
ametoa pongezi hizo katika salamu zake za mwisho wa mwaka ambapo
alisema kwamba, kwa mwaka 2017, Rais Magufuli ameweza kuiongoza nchi
vizuri kwa kudhibiti rushwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma.
Akitolea
ufafanuzi suala la makinikia, Seif alisema kuwa, Rais Magufuli ameweza
kupigania rasilimali za nchi hasa madini ili kuhakikisha wananchi wote
wanafaidika, hatua ambayo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kiongozi
huyo wa upinzani alisema, licha ya kuwa rushwa bado haijaisha, lakini
juhudi zilizofanywa haziwezi kubezwa kwani imepungua ikilinganishwa na
kipindi cha serikali ya awamu ya nne.
Pia,
aliwataka wanasiasa kutokuona shida kusifia mazuri ambayo yamefanywa na
serikali wakati wakifanya tathmini ya mwaka 2017. Seif alieleza namna
serikali ilivyowafikisha mahakamani vigogo wa rushwa, kurejesha nidhamu
ya fedha lakini pia kuokoa fedha zilizokuwa zikipotea kwa kuwalipa
watumishi hewa.
Mbali
na hayo, Seif pia alizungumzia changamoto za mwaka 2017 na kusema kuwa,
uhuru wa kufanya siasa nchini umebanwa kufuatia kuzuiwa kwa mikutano ya
kisiasa pamoja na maandamano.
Lakini
akielezea suala la Zanzibar, alisema, ubaguzi katika visiwa hivyo bado
ni changamoto kubwa kwani hata ajira zinatolewa kwa kufuata mrengo wa
kisiasa badala ya utaalamu wa mtu.
0 comments:
Post a Comment