Mwendesha
Mashitka wa Takukuru, Leornad Swai ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu kuwa mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi anayekabiliwa na kesi
ya utakatishaji fedha ameomba madaktari wake kutoka Afrika Kusini wawepo
wakati akifanyiwa upasuaji wa puto.
Pia
Swai ameeleza kuwa Mfanyabiashara James Rugemarila hana ugonjwa wa
saratani, pia na yeye ameomba madaktari wake kutoka India wawepo wakati
akiwa anafanyiwa uchunguzi.
Swai
ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi
hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa ambapo upelelezi bado
haujakamilika.
Wakili
Swai alieleza kuwa taarifa kuhusu afya za washtakiwa alizipata magereza
January 17, 2018 kama mahakama ilivyoamuru azifatilie.
Swai
alidai mshtakiwa Sethi anaishi na puto tumboni ambalo limeisha muda
wake, ambapo madaktari wa Muhimbili wamesema linatakiwa liondolewe.
Baada
ya kueleza hayo, Hakimu Simba alisema inaonekana madaktari wa Sethi
wameruhusiwa kuja nchini kumtibia, hivyo Magereza wafanye utaratibu kama
uliotumika kwa Sethi ili na Rugemarila atibiwe na madaktari wake.Kesi
imeahirishwa hadi February 2,2018.
Kwa
pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi,
utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60
na Sh.Bil 309.
0 comments:
Post a Comment