Kiongozi
wa chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe
amesema wanachama wa Chama hicho waliohamia Chama cha Mapinduzi (CCM)
sio kweli wanaunga mkono juhudi za Rais bali ni kwaajili ya madaraka na
ahadi walizopewa.
Hayo ameyasema jana kwenye hotuba yake kwa Kamati Kuu Juu ya chama hicho juu ya Hali ya Siasa Nchini Tanzania.
Mh.
Zitto alieleza kuwa hoja inayotolewa na wanachama wanaohama ACT
Wazalendo ya kuunga mkono jitihada za Rais haina mashiko kwani walikuwa
na nafasi ya kuunga mkono wakiwa ndani ya chama hicho.
"Takribani
watu wote wanaoondoka kutoka vyama vya upinzani kwenda chama tawala
wanasema wanaunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama Tawala katika
uendeshaji wa nchi yetu. Hii sababu haitoshi kueleza maamuzi yao,
hususani kwa wale wanaotoka chama chetu cha ACT Wazalendo", alisema Zitto.
Kiongozi
huyo wa Chama aliongeza kuwa Halmashauri Kuu ya Chama iliyooketi katika
ukumbi wa Jeshi la Wokovu, Aprili, 2016 iliazimia masuala ambayo chama
hicho kinaweza kuunga mkono ikiwemo mapamabno dhidi ya Ufisadi.
"Ni
dhahiri kuwa wenzetu wana sababu zaidi ya kumuunga mkono Rais, kuna
ambao sababu ni vyeo walivyopewa, na wengine ahadi za vyeo
watakavyopewa", alisema Zitto.
Chama
Cha ACT Wazalendo hivi karibuni kimeondokewa na wanachama wake
waandamizi ambao ni Profesa Kitila Mkumbo, Anna Mghwira, Albert Msando,
Samson Mwigamba na Edna Sunga. Wote wamejiunga na CCM.
0 comments:
Post a Comment