Nteghenjwa Hosseah, TAMISEMI.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amevitaka vituo vyote vya Afya Nchini sambamba na hospital
za Wilaya kutengeneza bustani ya kupumzikia kwa wagonjwa wanaosubiria
matibabu katika maeneo hayo.
Waziri
jafo ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya
katika Kituo cha Afya Makole kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka
uongozi wa Kituo hicho kutenegenza bustani ya kisasa pamoja na kupanda
miti ya kutosha ili kutunza matunzingira lakini kupendezesha eneo la
hospital.
“Hili
Agizo liende kwa Vituo vyote Nchini pamoja na Hospital za Wilaya
zilizoko chini ya TAMISEMI kuhakikisha wanaekeleza maelekezo haya katika
ameneo yote nataka hospital iwe sehemu ya kupa faraja mgonjwa kwa
kupata huduma nzuri lakini pia kusubiria huduma hiyo katika maeneo
yanayovutia wakati wote” Alisema Waziri Jafo.
Akikagua
majengo matano yanayojengwa katika Kituo hicho cha Afya na kusimamiwa
na TAMISEMI Waziri Jafo amesema ameridhishwa na Ujenzi wa miundombinu
hiyo ya Afya katika Hospital ya Makole kwani umefuata ramani
zilizotolewa na Wizara, unajengwa kwa ubora na uko ndani ya muda wa
Utekelezaji.
“Hivi
ndio ninavyotaka wataalamu wangu kujiongeza katika baadhi ya maeneo
mfano hapa Mmejenga Mabara kubwa kulingana na wingi wa wagonjwa
mnaowahudumia kwa siku sasa sio kwa sababu ramani imeonyesha maabara
ndogo basi kila mtu anafuata hivyo hivyo ni lazima tujiongeze kulingana
na mahitaji ya ameneo yetu ya huduma” Alisema Waziri Jafo.
Akizungumzia
maendeleo ya mradi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole amesema
Ujenzi huu umesema ujenzi wa Maabara, chumba cha Upasuaji, Wodi ya Kina
Mama, Nyumba ya Mganga pamoja na Ukarabati wa Kichomea Taka utakamilika
mapema mwezi February 2017 na Fedha zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi
huo zitatosha na kukamilisha ujenzi wa miundombinu yote.
Kituo
cha Afya Makole ni miongoni mwa vituo 211 Nchini
vilivyopokea/vitakavyopokea Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu
mbalimbali ya Afya lengo ikiwa ni kuboresha Miundombinu ya Afya ili
kuweza kutoa huduma bora kwa watanzania.
0 comments:
Post a Comment