Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole
amewazungumzia Askofu Zakaria Kakobe pamoja na baadhi ya viongozi
wengine wa dini na kusema kuwa hakuna mtu ambaye amezuiliwa kuongea
Tanzania na kuwa wapo huru kutoa maoni yao.
Polepole
alisema hayo juzi wakati akihojiwa na kituo kimoja cha Television na
kusema hakuna mtu ambaye ametishwa kwa kusema ukweli juu ya jambo fulani
ambalo huenda lipo au linatokea Tanzania.
"Hakuna
mtu amezuiliwa kuongea ukweli ndani ya nchi ya Tanzania, hakuna mtu
ametishwa kwa kusema ukweli na hasa katika uongozi wa awamu ya tano
chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, anayesema mtu Tanzania kuna mtu
kazuiliwa kuzungumza uhuru wake wa maoni nadhani atakuwa na matatizo ila
nachofahamu kwamba mtu kuzungumza lugha ya matusi kwa mujibu wa Katiba
yetu na sheria zetu ni makosa" alisema Polepole
Polepole
aliendelea kusisitiza kuwa viongozi hao wa dini wapo wazi na huru
kusema chochote kile kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
"Wapo huru kusema chochote kwa mujibu wa Katiba yetu ya nchi na sheria za nchi na nitasema neno moja dogo kitu ambacho na mimi ninatoa rai, nitakapokaa vizuri nitafafanua vizuri mambo haya lakini ukiwa kiongozi yoyote yule kauli ni jambo la msingi sababu una watu wanakufuata" alisisitiza Polepole

Juzi
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Mst. Projest
Rwegasira, ilitoa onyo na kuwataka viongozi wa jumuiya za kidini
kutotumia mahubiri yao ya ibada kwa kufanya uchambuzi wa masuala ya
siasa.
0 comments:
Post a Comment