Pacha
walioungana Maria na Consolata Mwakikuti wanaosoma mwaka wa kwanza Chuo
Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha (Rucu), wamelazwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Iringa kwa matibabu ya moyo.
Kaimu
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Alfred Mwakalebela amesema hali
zao zinaendelea vizuri ikilinganishwa na juzi walipofikishwa hapo.
Dk
Mwakalebela amesema leo Jumamosi Desemba 30,2017 kuwa pacha hao wapo
chini ya uangalizi wa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo.
“Wanaendelea vizuri tunamshukuru Mungu, tayari daktari bingwa wa moyo anaendelea kuwapa matibabu,” amesema Dk Mwakalebela.
Maria
na Consolata walijiunga na Rucu mwaka huu baada ya kuhitimu kidato cha
sita katika Shule ya Sekondari ya Udzungwa wilayani Kilolo mkoani
Iringa.
Wanalelewa
chini ya uangalizi wa Serikali ya Mkoa wa Iringa na Rucu kwa sasa.
Awali, walikuwa chini ya masista wa Shirika la Maria Consolata
lililowalea na kuwasomesha tangu wakiwa wadogo.
Na Tumaini Msowoya, Mwananchi
0 comments:
Post a Comment