Kiongozi
wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe
amekutana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa ajili ya kujadili
masuala ya uchaguzi wa haki nchini baada ya vyama hivyo kutangaza
kutoshiriki uchaguzi wa marudio.
Leo
December 21, 2107 Zitto amekutana na Mbowe ikiwa ni siku chache baada
ya kutoa taarifa kwamba watavizungukia vyama vyote vya siasa ili
kujadilia masuala ya uchaguzi.
Kwa
mujibu wa Afisa Habari wa chama hicho, Abdallah Hamis kikao cha chama
hicho kilichoketi hivi karibuni na kuamua kugomea kushiriki uchaguzi wa
marudio katika Kata na Majimbo mbalimbali nchini unaotarajiwa kufanyika
mapema mwakani.
“Kamati
Kuu ya ACT iliuagiza Uongozi wa Taifa wa Chama kuwafikia wadau wote wa
Demokrasia nchini na kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za
kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini kwetu, kwa
kuanzisha mazungumzo na vyama vyote vya Upinzani.
“Lengo
ni kuona njia bora zaidi ya mapambano ya pamoja ya kukabiliana na
vitendo vya chama tawala za kuvuruga chaguzi huru na za haki nchini,” –
Abdallah
Zitto
ameanza mazungumzo hayo na Mbowe, wakati Katibu Mkuu wa chama hicho,
Dorothy Semu, akiwa anaendelea na utaratibu rasmi wa kulitekeleza suala
hilo.
“Nilipewa
wajibu wa kuanzisha mazungumzo ya Viongozi wa Juu wa vyama, jana
nimezungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, ndugu James Mbatia
aliyeko hospitalini KCMC baada ya hapo nimekutana na Mbowe na kujadili
kuhusu mazingira ya chaguzi za haki nchini,”– Zitto
Aidha Zitto amesema mazungumzo na viongozi hao yameenda vizuri.
0 comments:
Post a Comment