kutoka
kwa jirani zetu Uganda kwa President Museveni ni issue ya Mwanaume
mmoja mwenye umri wa miaka 50, ambaye ni muuzaji wa vyakula
amethibitisha kwamba utajiri sio sababu ili uweze kuoa wanawake wengi.
Mohammed
Ssemada anayetoka katika kabila la Wagisu nchini Uganda amefunga ndoa
na wanawake wa tatu, Salmat Naluwugge, mwenye umri wa miaka 48 ambaye
ana watoto wa 5, dada yake Naluwugge ,Mastulah Nawanje 24, pamoja na
Jameo Nakayiza 27.
Harusi hiyo ilifanyika katika mji Wakiso huku umati wa watu walioshuhudia wakibaki mdomo wazi.
Kilichowashangaza
wengi ni kwamba mke wa kwanza Naliwugge ni mama wa watoto 5 na amekuwa
katika ndoa na Ssemada kwa muda wa miaka 20.
Ingawa
Ssemada amethibitisha kwamba yeye kipato chake ni cha chini ila
alionesha furaha kubwa kwa wake hao waliomkubali licha ya kipato chake
hicho duni.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao, Naluwugge alimshukuru Mungu kwa kuifanikisha harusi hiyo, ”Namshukuru mume wetu kwa kutuoa soote kwa siku 1. Kwangu, ni ishara tosha kwamba hatambagua yeyote”.
0 comments:
Post a Comment