Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wananchi
wa kijiji cha msosa kilichopo tarafa ya ruaha mbuyuni wameifukuza
kamati ya mipango na fedha kwa tuhuma za kufanya ubadhilifu wa mali za
kijiji na kuunda kamati mpya itakayoleta maendeleo katika kijiji hicho.
Wakizungumza
wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho wanachi
waliutaka uongozi wa kamati hiyo kuachia ngazi kutokana na tuhuma
zinazowakabili. Kwa
upande wake mtendaji wa kata MAIKO CHABILI ameafiki kuvuliwa madaraka
kwa viongozi wa kamati ya mipangano na fedha kutokana na tuhuma
zinazowakabili.
Hata
hivyo kamati ya mipango na fedha ya kijiji cha msosa walikubali
kujiudhuru na kulipa pesa ambazo ilibaini kuwa walizitumia vibaya bila
ruhusa ya wananchi.
mtendaji
wa kata ya Ruaha Mbuyuni Maiko Chabili akiwafafanulia jambo wananchi wa
kijiji wakati wa mkutano wa hadhara ulikuwa na lengo la kuwafukuza
kamati ya mipango na fedha ya kijiji kwa matumizi mabaya ya pesa zao
0 comments:
Post a Comment