Sehemu ulimokuwa umefukiwa mwili wa Marehemu baada ya kufukuliwa
Dada wa marehemu akizungumza na mwandishi wetu
Shemeji wa Marehemu akizungumza na wamdishi wetu
Eneo
hili alilokuwa amezikwa marehemu, imeelezwa mtuhumiwa alipindisha
mfereji wa maji upitejuu ya alimofukiwa marehemu kama njia mojawapo ya
kupoteza ushahidi
Muonekano wa nyasi zilivyokuwa kabla ya kufukua kuutoa mwili wa marehemu
Baada ya kumfukua hapa ndipo alipozikwa upya marehemu kwa heshima zote
Safari ya Mwandishi wetu na shemeji wa Marehemu kuelekea eneo la tukio
Mke wa Mtuhumiwa wa mauaji hayo akizungumza na mwandishi wetu
Akisimulia mkasa huo huku akiwa na majonzi
makubwa dada wa marehemu Bi Marry Tweve
amesema mnamo mwaka 2012 familia ilianza kumtafuta baada ya kutoonekana
kijijini hapo Igolwa Wilaya Makete mkoa wa Njombe bila mafanikio huku wakiamini
ndugu yao yupo kufanya kazi ya kupasua mbao eneo la Matema kabla ya kuanza kupata taarifa za awali za
marehemu kuuawa na kuzikwa mtoni na rafiki yake ambaye awali walikuwa wakifanya
kazi ya kupasua mbao pamoja katika maeneo tofauti tofauti
Bi Marry amesema walianza kupata taarifa za marehemu kuuawa na kuzikwa
Oktoba mwaka huu na wao kama familia walitoa
taarifa kwenye vyombo vya dola ili kumtia nguvuni mtuhumiwa na kuongeza kuwa baada
ya mtuhumiwa kukamatwa na vyombo vya dola mtuhumiwa alikiri kumuua marehemu kwa
kumkata panga kisogoni na kwenda kuonesha eneo alilomfukia kabla ya polisi
kuamuru mwili huo kufukuliwa kwa uchunguzi zaidi na kuzikwa upya
Katika eneo la tukio baada ya kufukuliwa mwili wa
marehemu ulikuwa tayari umekwisha oza na kubaki mifupa mitupu lakini
zilionekana nguo zake pamoja na panga linalodaiwa kutumika katika mauaji hayo,
ambapo mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika pekeyake kutekeleza mauaji hayo
Baada ya mwili wa
marehemu kufukuliwa na kuzikwa tena kwa taratibu zote Bi Marry amelishukuru
jeshi la polisi wilaya ya Makete kwa kushirikana pamoja na familia kufanikisha kumtia
nguvuni mtuhumiwa na kuviomba vyombo vya
dola (polisi na mahakama) kutenda haki ili iwe fundisho kwa wanajamii wenye
tabia kama hizo
Mwandishi wa habari hii haikuishia hapo, alifunga
safari ya umbali wa kama kilomita 4
kwenda eneo ambalo mwili wa marehemu ulizikwa awali na mtuhumiwa (umbali
wa mita kama mia tisa) kutoka katika barabara ya Igolwa Ikwenzulu pembezoni mwa mto na kushuhudia mahali ambapo
marehemu alizikwa kabla ya kufukuliwa kwa kuongozana na shemeji wa marehemu Tm
Wiliamu Tweve
Amesema baada ya mwili huo kufukuliwa sehemu ya
mabaki ya mwili wake yalichukuliwa (fuvu na mfupa wa paja) kwa ajili ya
uchunguzi zaidi na mabaki mengine ya mwili huo yalizikwa upya eneo lingine
lililotengwa na familia katika shamba lililopo jirani na alipokuwa amefukiwa
awali
Mke wa mtuhumiwa anayedaiwa kufanya tukio hilo amezungumza
na mwandishi wetu na kusema hakufahamu kama mumewe alitenda kosa hilo miaka
yote hiyo imepita na anajisikia vibaya kwa kitendo hicho kilichofanywa na
mumewe
Amesema jamii imemuelewa kuwa yeye hakushirikiana
na mumewe kutenda kosa hilo, na mahusiano yake na jamii ni mazuri
Mtuhumiwa huyo kwa sasa anashikiliwa na vyombo
vya sheria kwa hatua zaidi za kisheria
0 comments:
Post a Comment