Spika
wa Bunge, Job Ndugai amekosoa mpango wa TAMISEMI kuwapangia walimu
wapya vituo vya kazi moja kwa moja akisema kazi hiyo ni ya Halmashauri
kwani ndizo zinazofahamu maeneo yenye uhaba wa walimu.
Ndugai
amesema hayo leo Jumamosi Desemba 23,2017 ikiwa ni siku moja baada
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo kutangaza majina ya
walimu wapya 3,033 waliopangiwa vituo vya kazi.
Katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dodoma, Ndugai amehoji Tamisemi ni nani hata aweze kujua ikama ya walimu shuleni.
Amesema wamekuwa wakijaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji na kuyaach maeneo yenye uhitaji.
“Jambo
hili linakera, kila mahali sasa ni Tamisemi hadi napata shaka, hivi hii
zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au
ndiyo kupoka madaraka kwa wengine?” alihoji Ndugai.
Akitoa
mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa, Ndugai alisema ina
wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya
sayansi hata siku moja.
“Juzi
mmepanga walimu na nilipita tena hapo hakuna hata mwalimu. Hawajasoma
hesabu, fizikia, baiolojia, kemia na jiografia; nauliza tena wanasema
Tamisemi, hivi hao walisoma wapi na ninyi mmesoma shule zipi?” alihoji
na kuwasihi wabunge wa Mkoa wa Dodoma kuwa wanatakiwa kuupinga mpango
huo bungeni wakati yeye akiongoza vikao vya Bunge.
Aidha,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wote
wa wilaya kuangalia ikama ya walimu na kuwatawanya vituoni mara moja.
0 comments:
Post a Comment