Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa kuna haja kubwa ya
kuyafanyia uchanguzi makanisa ili kuweza kujua makanisa halisi ili
kuweza kutofatisha na mawakala wa shetani.
Ameyasema
hayo jijini Arusha ambapo amesema kuwa baadhi ya makanisa yamekuwa
yakiwapotosha wananchi kwa kuwajaza imani isiyokuwa ya kibinadamu.
Amesema
kuwa historia ya mchungaji Kakobe inatia mashaka kwani amebeba vyeo
vyote vya kanisa hata anaposafiri huwawekea waumini wake ‘Cassete’ ili
wamsikilize akiwa safarini.
“Kuna
watu wengine ni mawakala wa shetani, hivyo kuna kila haja ya kuanza
kufanya uchambuzi wa makanisa haya ambayo yamekuwa yakipotosha
Watanzania, unaofanywa na anayejiita Askofu Kakobe ni umburula,”amesema
Gambo
Hata hivyo, ameongeza kuwa taasisi ya dini ina utaratibu wake inaheshimika, ina mfumo wake na inathaminika katika jamii.
0 comments:
Post a Comment