Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amekaa mwenyewe pasipo
msaada wa madaktari katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya,
anakotibiwa baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake, Area D,
Dodoma huku hali yake ikizidi kuimarika kila kukicha.
Desemba
26, mbunge huyo alisimama kwa mara ya kwanza na kuanza rasmi kufanya
mazoezi ya viungo katika Hospitali hiyo kwa msaada wa madaktari. Lissu
anaendelea na mazoezi madogo ya kuimarisha misuli ya miguuni ili aweze
kutembea.
Akielezea
hali yake, Mhe. Tundu Lissu amesema kwa sasa anauwezo wa kukaa bila
kuegemea kwenye kitu chochote, hali ambayo awali alikuwa anashindwa
kufanya hivyo.
“Ninawashukuru kwa sala na maombi yenu. Sasa ninaweza kukaa bila ya kuegemea kitu.“ameandika Mhe. Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Mwanasheria
mkuu huyo wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya
gari mara baada ya kufika nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7,
hivi karibuni alisema bado ana risasi moja mwilini mwake ambayo
haijatolewa.
0 comments:
Post a Comment