Tanga.
Matukio
ya utekaji na uporaji katika jiji la Tanga,yanazidi kuwapa hofu
wananchi baada ya dereva mmoja wa bajaji,Fadhil Abubakar (20) kukutwa
amekufa kwa kunyongwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni abiria waliokuwa
wamemkodi.
Akizungumza
leo Jumapili Desemba 24, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Edward
Bukombe amesema mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia jana katika eneo
la Kona Z kata ya Kiomoni Tarafa ya Chumbageni.
Watu
waliozungumza na gazeti hili kuhusiana na mauaji hayo, wamesema
walianza kukusanyika katika eneo la Kona Z baada ya kupata taarifa
kutoka kwa askari wa jeshi la Wananchi JWTZ kikosi cha Pande waliokuwa
wakikimbia mchakamchaka alfajiri ya kuamkia juzi.
“Askari
waliokuwa katika mchakamchaka asubuhi walipofika eneo la Kona Z wakaona
mwili wa mtu aliyekufa ndipo wakatoa taarifa na sisi tukakusanyika
kushuhudia”amesema Said Jumaa mkazi wa Kona Z.
Kamanda
Bukombe amesema Fadhili alikodiwa na abiria juzi usiku waliotaka
kupelekwa kijiji cha Pande na baada ya hapo hakuonekana tena.
“Alikodiwa
na abiria walioomba kupelekwa kijiji cha Pande na walipofika Kona Z
wakamnyonga kwa kamba ya katani kisha wakampora bajaji aliyokuwa
akiendesha na kumtupa kwenye kichaka kilichopo kando ya barabara,”
amesema Bukombe.
Amesema
kituo alichokuwa akiwasubira abiria amerehemu kipo barabara ya 10
karibu na hoteli ya Asad na kwamba aliondoka saa 3.00 usiku na kupitia
nyumbani kwa kaka yake barabara ya saba ambako alimuaga kuwa anakwenda
nyumbani kwake Magomeni kulala.
“Baada
ya hapo hakuonekana tena hadi askari wa JWTZ walipouona mwili wake
ukiwa umetupwa kwenye kichaka kando ya barabara ya Amboni-Pande”amesema
na kubainisha kwamba Polisi linawasaka waliohusika na mauaji hayo.
0 comments:
Post a Comment