Ikiwa leo Wakristo duniani kote wanaadhimisha sikukuu ya Krismas, Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Chemba amewataka Watanzania kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa Amani na Upendo
Waziri
Mwigulu ambaye wizara yake ndio ina dhamana ya kusimamia amani na
usalama wa raia na mali zao nchini ametoa salamu zake za sikukuu huku
akiwakumbusha wananchi kuzingatia Amani.
Kupitia
Ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Mh Mwigulu ameandika, “Merry
Christmass & Happy New Year, tusherekee kwa Amani na Upendo”.
Mbali
na Waziri Mwigulu kusisitiza Amani kipindi hiki cha sikukuu, hivi
karibuni pia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro aliwataka
Watanzania kusherehekea sikukuu bila kuvunja sheria za nchi.
0 comments:
Post a Comment