Mbunge
wa wa Tarime John Heche amewaonya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuwa
kama wanataka kumjibu Askofu Zacharia Kakobe kwa niaba ya serikali
iliyopo madarakani basi wajibu kwa hoja na siyo kuropoka
Heche
amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi mkoa huo, Frank Kamugisha kumtaka Askofu Kakobe aende kufanya
toba na kisha kuwaomba radhi wana CCM wa Dar es salaam kwa kuacha miiko
ya kidini na kushindwa kutumia busara na kisha kusema hovyo.
Akizungumza
jana na Wanahabari Kamugisha alivitaka vyombo vinavyohusika na sheria
vihakikishe hakuna mtu anayepata fursa ya kumtukana au kumbeza Rais wa
nchi na kufafanua kwamba Rais amejipambanua katika kuwasaidia wananchi
na anafanya mambo hayo kwa udhati wa moyo wake hivyo mtu anyebeza moja
kwa moja atakuwa msaliti.
Heche amandika kwenye ukurasa wake wa Twitter na kusema kwamba "CCM
kama mnataka kujibu hoja za Askofu Kakobe kwa niaba ya Rais Magufuli na
Serikali jibuni kwa hoja, sio kuropoka! kazi za wachungaji ni kukemea
maovu yote yaliyopo duniani, watu wanapotea, wanapigwa risasi,
wanaokotwa baharini, sheria za nchi hazifuatwi, haya yatakemewa na kila
mtanzania" Heche.
0 comments:
Post a Comment