Mrisho
Gambo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na baadhi ya walimu wa shule ya
Embarway Sekondari iliyopo Arusha na kusema kama walimu Wakuu
wakifanya utaratibu mzuri itasaidia walimu hao kunufaika na fursa
mbalimbali kwa usawa, jambo ambalo litasaidia kuondoa upendeleo.
"Kumekuwepo
na malalamiko sehemu zingine kwenye zoezi kama la leo hili la kusimamia
mitihani unakuta kila mwaka wanakwenda walimu wale wale rafiki zake
Mkuu wa shule, kama wewe kiwango chako cha kujipendekeza ni kidogo wewe
utakuwa unasikia kwa wengine tu maana orodha ya walimu wanaokwenda
kwenye usimamizi huwa inapagwa na Mkuu wa Shule, maeneo mengine nasikia
wanaangalia sana jinsi kama ni mdada akimpa ushirikiano zaidi Mkuu wa
Shule huyo dada hakosi lakini tumekuwa tukisisitiza hiyo kazi ya
kusimamia mitihani ni kazi ya kila mwalimu" alisema Gambo
Aliendelea kufafanua kuwa "Kwa
Mkuu wa shule anayejitambua anapaswa kutengeneza utaratibu mzuri ili
kuwe na mzunguko, kila mwalimu mwenye sifa aweze kushiriki kwenye zoezi
hilo, haiwezekani ukaenda kila mwaka, unaweza kwenda mwaka huu mwakani
akaenda mwingine, baadaye ikafika tena zamu yako. Kwa sababu walimu hawa
hawana kazi ya ziada, ofisi zingine wanalipwa masaa ya ziada lakini
walimu hawalipwi, mwalimu hana posho, mwalimu hana safari, mwalimu yeye
ni mitihani, sensa na kusimamia uchaguzi basi sasa hizo fursa zinapaswa
kuwekewa utaratibu mzuri ili kila mmoja anufaike nazo
0 comments:
Post a Comment