Mbunge
wa jimbo la Makete Profesa Norman Adamson Sigara King ametoa machango wa bati
150 ikiwa ni kuchangia ujenzi wa madarasa na nyomba ya mwalimu ktika shule ya sekondary
isapulano inayotarajiwa kuanza rasmi tarehe 8 januali 2018.
Akiongea
na wananchi wa kata ya isapulano Mh.sigara amewapongeza wananchi kwakujitolea nguvu zao kujenga shule hadi
kufikia hatua ya kupata usajili ambapo amesema tayali shule hiyo ieshapangiwa
wanafuzi 40.
Katika
hatua nyingine mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya makete
bw,fransic namaumbo masema kupata usajili wa shule kunategemea ushirikiano wa wananchi
na serkali pamoja na wadau wengine kwakuwa ujenzi wa shule unahitaji nguvu
kazi,raslimali fedha,pamoja mamlaka husika.
Kwaupande
wake diwani wa ata ya isapulano ametoa pongezi zadhati kwa prof sigara kwa
mchango wake wa fedha kiasi cha million moja kwaajili ya saruji kumalizia
umaliziaji wa maabara na mabati 150 pamoja na juhudi za kuhakikisha shule
inapewa usajili.
Aidha
wananchi wa kata ya Isapulano wamemshukuru Mh.Mbunge kwa mchango wake huku
wakirudisha matumaini ya kuondoka katika adha ya kusafiri umbali mrefu kupeleka
watoto shule ambapo kwasasa wana safili zaidi ya kilometa mpaka 20 kupeleka
watoto shule.
0 comments:
Post a Comment