Baadhi
ya wazazi na walezi wa kata ya isaplano
wilayani makete mkoani njombe wamesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwapeleka
watoto shuleni kwani ni haki ya mtoto kisheria huku wakitoa wito kwa wazazi
wengine kuwapeleka watoto shule ili kuongeza watalamu mbalimbali hapa nchini.
Wakizungumza
na AM BLOG wananchi hao wamesema kuwa
kumpeleka mtoto shule kuna mjengea uwezo wa kutambua fursa mbalimbali za
kimaendeleo ili kuwa na taifa ambalo lina wasomi wengi ambao wataleta chachu ya
maendeleo katika taifa
Katika
hatua nyingine wananchi hao wameiomba serikali kuchukua hatuka kali za kisheria
kwa wazazi ambao hawata wapeleka watoto shule ili iwefundisho kwa wengine kwani
kuna baadhi ya wazazi huwa hawataki kuwapeleka watoto shule kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo changamoto za kiuchumi.
WAKATI
HUO HUO
Kutokana
na changamoto ya ubovu wa barabara ya kutoaka luvulunge mpka isaplano wananchi
wa kata ya isaplano wamesema barabara hiyo inakwamisha shughuli mbalimbali za
kimaendeleo katani hapo ikiwemo kushindwa kusafirisha mazao yao kwa ajiri ya
biashara jambo ambalo linapelekea wananchi na kushindwa kujikimu kataka maisha.
0 comments:
Post a Comment