Licha
ya Jeshi la polisi mkoa wa kusini Unguja kupambana na ajali za
barabarani bado madereva wanaendelea kupoteza maisha ya watu na
kuwaachia majeraha kufuatia ajali ya Gari Aina ya haise kugongana na
Gari ya jeshi la wananchi wa Tanzania huko kidimni wilaya Ya kati mkoa
wa Kusini unguja .
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja Makarani
Khamis Ahmed amesema kuwa ajali hiyo iliyotokea asubuhii ya Leo
iliyohusisha Gari ya abiria aina ya haise yenye Namba za usajili Z. 675
roti namba 227 Machui imeigonga gari Ya jeshi la wananchi Tanzania yenye
Namba 5937 JW12.
Ameongeza
kusema chanzo cha ajali hiyo kuwa dereva wa Gari ya abiria ameshindwa
kuchukua tahadhari za msingi kabla Ya kuingia kwenye barabara kuu na
ndipo alipotoka na kuigonga gari ya jeshi la wananchi wa Tanzania .
Kamanda
Makarani ametoa wito kwa madereva wa magari Ya abiria pamoja na magari
mengine wanapoingia kwenye barabara wachukue tahadhari na kuwa makini
pamoja na kuheshimu sheria na kanuni za barabara ili kuepuka ajali
zinazoweza kuepukika.
0 comments:
Post a Comment