Home » » Dereva wa basi la mwendokasi asimamishwa kazi baada ya kunaswa akijisaidia mlangoni

Dereva wa basi la mwendokasi asimamishwa kazi baada ya kunaswa akijisaidia mlangoni

Unknown | Sunday, December 24, 2017 | 0 comments
Dereva mmoja wa basi la nwendokasi la Kampuni ya Gold Coast nchini Australia amejikuta akisimamishwa kazi baada ya video yake kuvuja ikimuosha akijisaidia haja ndogo mlangoni mwa basi hilo


Kamera hizo zilimnasa dereva huyo akiwa mlangoni akijisadia haja ndogo bila kujua kama anarekodiwa na baadaye kuingia ndani ya gari ambalo ndani kulikuwa na abiria wawili pekee.
Taarifa kutoka mtandao wa 9 News umeeleza kuwa dereva huyo baada ya video hiyo kuvuja tayari ameshasimamishwa kazi .
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ndiye alirekodi tukio video hiyo ameeleza kuwa alifanya hivyo kama makusudi baada ya wiki kadhaa kampuni hiyo kulaumiwa na wateja kuwa madereva wa kampuni hiyo hawana nidhamu.
Watu wamekuwa wakiilaumu Kampuni hii kila siku kuwa madereva wao hawana nidhamu wiki mbili zilizopita kuna dereva alitupa chupa ya plastic iliyokuwa na maji machafu yenye asili ya mkojo lakini kampuni baada ya tukio hilo haikufanya lolote na ndio maana ni karekodi na tukio hili.“amesema shuhuda aliyerekodi tukio hilo aliyejulikana kwa jina moja la Frank kwenye mahojiano yake na 9 News .
Hata hivyo uongozi wa Kampuni hiyo tayari umeshatangaza kumfuta kazi dereva huyo ambaye hawajamtaja jina lake.
Tumeiona video hiyo na muhusika tumesha msimamisha kazi kwa ajili ya kupisha uchunguzi, Tunajua matukio haya ni mabaya kwenye jamii na kwa kampuni yetu hivyo kama itakuwa ni kweli muhusika tutamchukulia hatua za kinidhamu zaidi.“ameeleza msemaji mkuu wa Kampuni ya Gold Coast.
Tukio hilo limetokea jana  jumamosi na dereva huyo imeelezwa kuwa ni Mchina na alikuwa a
Tazama video ya tukio hilo kama ilivyorekodiwa na mtandao wa 9 NEWS.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG