Kuna mti mmoja (jina lake linahifadhiwa ) unapatikana porini, mti huo ukikomaa, urefu wake hauzidi wa mtoto wa miaka saba, una magamba kwa mbali na rangi yake ni nyeupe
Mti huu ukikauka ukausaga unga wake huwa mweupe kama mti wenyewe.
Ukichukua unga wa mti huu halafu ukajipaka usoni unakuwa na uwezo wa kuwaona wachawi na misukule.
Ukijipaka unga wa mti huu usoni halafu ukatembea mtaani wakati wa mchana, unaweza kuona mambo yote yanayofanyika katika siri kubwa kama vile wachawi wakiwa wanawanga au wanafanya shughuli zao wakiwa uchi.
Mti huu unakufanya pia kuwa na uwezo wa kuwaona misukule na kama wewe ni mfanyabiashara ya duka basi mti huu utakupa uwezo wa kuwaona watu wanao kuja dukani kwako na hela za chuma ulete.
Vilevile mti huu una uwezo wa kukimbiza nyoka mfano ukiwa na kipande cha mti huu mfukoni halafu ukawa unatembea, kama mbele yako kuna nyoka atakimbia kabla hujafika.
Pia mti huu hutumiwa na watu wanao fanya shughuli ya kutafuta mali zenye asili ya kukaliwa, kushikiliwa,kulindwa na kufichwa na majini wa kisheitwani kama vile madini na mali mbalimbali.
Kwa ufupi mti huu unakaliwa na majini ambao kazi yao kuu ni kufunua mambo yaliyowekwa sirini na kufichua mambo yote yaliyofichwa.
Kwa hiyo mtu akichanjiwa ama kupakwa uchawi huu anakuwa na uwezo wa kuona mambo yaliyo fichwa na kuwekwa sirini.
MTI MWEUPE WA KUONA WACHAWI NA ULOZI KATIKA MAPENZI.
Mti mweupe una matumizi mengi sana. Moja kati ya matumizi hayo ni pamoja na kutumika katika ulozi wa mapenzi.
Katika ulozi wa mapenzi, mti mweupe hutumika Zaidi katika uchawi wa mapenzi ambao hutupwa kwa njia ya kumtegea mtu kwenye njia anayo itumia kupita.
Kama unataka kumtega mtu ulozi wa mapenzi, basi usiku utachukua huu mti mweupe kiasi utajipaka usoni, kiasi utaufunga kwenye kitambaa chekundu na kuweka chini ya mto ambao utaulalia na kiasi utachoma kwenye koroboi au chetezo huku ukimnuizia mtu ulie mkusudia na kuwaomba majini wanao husiana na mti huu mweupe wakufunulie na kukuonyesha njia ambayo mtu ulie mkusudia atapita kesho yake au katika siku maalumu ya kinyota ambayo umepanga kumtega mtu huyo uchawi huo wa mapenzi.
Usiku wa siku hiyo utamuona katika ndoto mtu ulie mkusudia akipita katika njia ambayo wewe unaifahamu.
Ikifika kesho yake asubuhi utatakiwa kwenda katika njia hiyo na kutega dawa nyingine ya ulozi wa mapenzi ambayo hutumika kwa kumtega mtu aruke ili imnase.
Na mtu huyo akisharuka katika njia hiyo basi dawa itamnasa na jinni wa mapenzi aliekusudiwa atamuingia mtu huyo na kuamuru kufanya mambo yote ambayo mlogaji alikusudia kuyafanya.
Hivyo ndivyo mti mweupe wa kuona wachawi unavyo tumika katika ulozi wa mapenzi.
Mbali na kutumika katika ulozi wa mapenzi mti huu unatumika katika mambo mengine mengi sana mazuri kwa mabaya.
Mambo yote hayo utayapata kuyafahamu kupitia kitabu changu ambacho kitatoka mwezi wa saba kati kati. Kitabu hicho kinaitwa : MAMBO TISA YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU NA UHUSIANO KATI YA NYOTA YA MTU NA MAFANIKIO YAKE KATIKA MAISHA ambacho kimeandikwa nami DOKTA. MUNGWA KABILI.
Ndani ya kitabu hiki utapata kufahamu kila kitu kuhusu mti mweupe, kuanzia taratibu za kuuchukua porini, siku na muda unao takiwa kuuchukua porini, maneno unayo takiwa kuyatamka wakati unauchukua mti huu porini, masharti ya kutumia mti huu, jinsi unavyo weza kujiepusha na shari za wachawi na walozi zitokanazo na kuutumia mti huu pamoja na matumizi yote ya mti huu kuanzia kujipaka, kuchanjiwa,kuchoma, kufukiza, kupuliza pamoja na mambo yoote yanayo husiana na mti huu.
Maelezo kuhusu kitabu hiki yanapatikana :http://mungwakabhili.blogspot.com/2018/06/mambo-tisa-yanayo-unda-nyota-ya.html
MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI. ANAPATIKANA KWA SIMU NAMBA 0744 000 473.
2 comments:
ahsant sana doctor,naombunisaidie kunitumia picha ya mti huo,wats app yangu +25769481868,,ninaomba kuona mchawi ambae analala juu ya nyumbayangu,asante
Baada ya kuona chapisho kwenye mtandao la Jenna kutoka USA akisema jinsi alivyosaidiwa na Dk. DAWN, niliamua pia kuwasiliana naye kwa msaada kwa sababu sikuwa na chaguo nilichotaka ni kumrudisha mpenzi wangu na furaha. Kwa mshangao mkubwa mpenzi wangu alifika nyumbani akiwa amepiga magoti kwamba nitafute nafasi moyoni mwangu kumsamehe, hakika nilistaajabu na kushtuka mpenzi wangu alipopiga magoti akiomba msamaha na mimi nimkubalie tena. Kweli nimepungukiwa na maneno, na sijui ni kiasi gani cha kukushukuru wewe Dr. DAWN. Wewe ni Mungu aliyetumwa kurejesha uhusiano uliovunjika, Na sasa mimi ni mwanamke mwenye furaha. mawasiliano yake ni Whatsapp +2349046229159
Post a Comment