Home » » Udart kuhamisha ofisi Jangwani, wafanyakazi wapewa likizo

Udart kuhamisha ofisi Jangwani, wafanyakazi wapewa likizo

Unknown | Monday, May 07, 2018 | 0 comments
Mabasi 29 ya mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart) yameharibika kutokana na eneo lake la maegesho kujaa maji yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini hapa.

Maegesho ya mabasi hayo yaliyopo eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam hujaa maji kila inaponyesha mvua kubwa.

Mbali ya mabasi, pia baadhi ya wafanyakazi wamepewa likizo mpaka maegesho mengine ya mabasi hayo yatakapopatikana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 7, 2018 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Udart, Deus Bugaywa amesema kujaa kwa maji eneo hilo kumesababisha shughuli mbalimbali kusimama jambo lililowafanya waanze kutafuta eneo lingine la kufanyia kazi.

Amesema moja ya sababu iliyochangia hali hiyo ni sehemu ya ukuta ya eneo hilo kudondoka na hivyo maji ya Mto Msimbazi kuingia ndani kwa wingi.

Amesema matengenezo ya mabasi hayo yanafanyika eneo la maegesho ya muda katika vituo vyao vya Gerezani, Kivukoni na Kimara wakati wakiendelea kutafuta sehemu nyingine.

Advertisement
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG