Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa
TAKUKURU Mkoa wa Njombe imeokoa kiasi cha Shilingi Milioni kumi na moja
zilizokuwa zitumike tofauti na Matarajio kwenye Ujenzi wa Zahanati ya Itambo
Wilayani Wanging’ombe
Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Njombe CHARLES
NAKEMBETWA akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake hii leo amesema
mradi huo uliofadhiliwa na Ubalozi wa JAPAN kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na
kutengewa fedha zaidi ya Milioni mia saba ulioratibiwa na kusimamiwa na NG’O ya
MSETI DEVELOPMENT ASSOCIATION ya Mjini Njombe
Hata hivyo pamoja na kulipwa fedha zote
Kamanda huyo amesema kampuni hiyo haikuweza kukamilisha mradi huo kwa
wakati hivyo TAKUKURU baada ya kupata taarifa
ilianza kufanya uchunguzi na kubaini tatizo kwenye mradi huo
Pia afisa huyo wa TAKUKURU amesema fedha hizo
zilizookolewa zitakabidhiwa katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Njombe
aliyekuwa Msimamizi wa Mradi huo ili ziweze kufanya kazi ya ujenzi wa Zahanati
husika
Na uchunguzi utakapokamilika wahusika
watafikishwa Mahakamani
0 comments:
Post a Comment