Wanafunzi Shule ya Msingi Luvulunge iliyopo
kata ya Isapulano Wilayani Makete wameanza kunufaika na Elimu ya wasaidizi wa Kisheria
inayotolewa na Shirika la Makete Paralegal Organisation(MAPAO)
Mkurugenzi wa Shirika hilo la Wasaidizi wa
Kisheria Wilaya ya Makete DENIS SINENE amesema utoaji wa Elimu hiyo kwa
Wanafunzi ni katika kuwasaidia watoto kuwa na Misingi bora ya Elimu na kujua
haki zao za Msingi ikiwa ni pamoja na wao kutambua wajibu wao
Mkurugenzi wa Shirika hilo la Wasaidizi wa
Kisheria Wilaya ya Makete DENIS SINENE Ametoa Maelezo hayo wakati wa kuanzisha
Klabu ya Wasaidizi Shuleni hapo ikiwa ni Mwendelezo wa kuanzisha Klabu hizo
kwenye Shule za Sekondari na Msingi Wilayani hapa
Mkurugenzi huyo ameelezea dhamira na Lengo la
kuwepo kwa Wasaidizi wa Kisheria Wilayani hapa pamoja na kuwataka watoto kuwa
watiifu kwa wazazi wao na Jamii inayowazunguka
Kwa Upande wake Mjumbe wa Bodi ya MAPAO
amesema wanafunzi hao wakiendelea kupatiwa Elimu hiyo mara kwa mara Taifa
litakuja kuwa na Vijana waadilifu na kuyaishi mema wakati wote
Mkurugenzi wa Shirika hilo la Wasaidizi wa
Kisheria Wilaya ya Makete DENIS SINENE amesema watoto wanatakiwa kujitambua kwa
kujua wajibu wao kwa wazazi huku Klabu ya wasaidizi wa Kisheria iliyoundwa hii
leo shuleni hapo ikiwa na wajumbe Zaidi ya 40
Shirika la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya
Makete MAPAO linaanzisha Klabu 2 za Wasaidizi wa Kisheria kwa Wanafunzi moja
kutoka shule ya Sekondari Iwawa na Klabu nyingine imeanzishwa leo shule ya
Msingi Luvulunge na leo ni kuendelea kutoa Elimu ya Kisheria kwa wanafunzi shule
zote za Msingi na Sekondari Wilayani hapa
0 comments:
Post a Comment