Home » » Waziri: ''TFF haipo juu ya Serikali....Tunawajibu wa Kuisimamia"

Waziri: ''TFF haipo juu ya Serikali....Tunawajibu wa Kuisimamia"

Unknown | Thursday, April 12, 2018 | 0 comments
Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Juliana Shonza imesema Shirikisho la soka nchini TFF limesajiliwa chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano hivyo shughuli zake zote zipo chini ya serikali.

Mh. Shonza ameyasema hayo jana wakati akjibu swali la mbunge wa Singida Mjini Mussa Ramashani Sima ambaye alihoji kuhusu mamlaka ya Waziri katika kusimamia kazi za TFF ikiwemo mapato na matumizi ya shirikisho hilo kutokana na katiba ya TFF kutoruhusu kuingiliwa na serikali.

''TFF pamoja na viongozi wake wote, wanapaswa wanalazimika na hivyo wanatambua mamlaka ya Waziri, kwasababu katiba ya TFF inatambua kuwa TFF ni chombo cha mpira ambacho kimesajiliwa chini ya sheria ya Baraza la Michezo ya 1967 na marekebisho yake ya mwaka 1971'', alisema Shonza.

Aidha Mbunge Mussa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Singida amemuomba Waziri kuhakikisha wanaibana TFF ili ipeleka mpango kazi kwenye vyama vya mikoa ili kujua matumizi ya pesa za ruzuku zinazotolewa kwa shirikisho hilo.

Advertisement
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG