WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Bw.
Stephen Mafipa kumtafuta popote alipo na kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Bw. Fortunatus Kagoro kwa tuhuma za
matumizi mabaya ya fedha.
Mbali
na Bw. Kagoro pia Kaimu Mweka Hazina Bw. Heri Hamad Afisa Mipango Bi
Teresia Nsumba nao ameagiza wakamatwe na baada ya uchunguzi
watakaobainika kwamba hawajahusika na ubadhilifu huo watarudishwa
kazini. "Lazima fedha za Serikali zitumike kama ilivyokusudiwa."
Watendaji
hao wanadaiwa kutumia sh. bilioni 1.8 zilizotolewa na Serikali kwa
ajili ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa kuchora
mchoro na kujenga msingi katika maeneo mawili tofauti.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati
akizungumza na watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Masasi na
Halmashauri ya wilaya ya Masasi akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani
Mtwara.
Amesema
mwaka 2014 Serikali ilipeleka sh milioni 575 wilaya Masasi kwa ajili
ya ujenzi wa jengo la Halmashauri hiyo na fedha hizo ziliishia kutumika
katika hatua za maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kutengeneza
michoro ya jengo.
Waziri
Mkuu amesema 2016/2017 Serikali ilipeleka tena sh. bilioni 1.25 kwa
ajili ya ujenzi huo, ambapo Halmashauri hiyo ilienda kutafuta eneo
lingine na kufanya tena shughuli zilizokuwa zimefanyika na kuanza ujenzi
ambao umeishia katika msingi na fedha zimeisha.
Pia
amewataka watendaji hao kutotumia fedha za makusanyo ya ndani kwa ajili
ya kuziba pengo la fedha za mradi huo ambazo baadhi yake hazijulikani
zilipo na amewaagiza Madiwani kutoruhusu jambo hilo.
"Madiwani
msikubali kutumia fedha za makusanyo ya ndani kupeleka kwenye ujenzi wa
miradi ya maendeleo ambayo tayari Serikali ilishatoa fedha ya ujenzi
wake.
Amesema
Serikali inahitaji kuona fedha za maendeleo zinazopelekwa katika
Halmashauri mbalimbali nchini zinatumika kama ilivyoelekeza na si
vinginevyo na Serikai haitakuwa na mzaha kwa mtumishi atakayezitumia
vibaya.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 26, 2018.
0 comments:
Post a Comment