Home » » WANAUME MAKETE WAHIMIZWA KUFANYIWA TOHARA

WANAUME MAKETE WAHIMIZWA KUFANYIWA TOHARA

Unknown | Monday, February 26, 2018 | 0 comments
Daktari Jonathan Kitundu
Wanaume Wilayani Makete Mkoani Njombe wamehimizwa  kujitokeza kwa wingi kufanyiwa Tohara ili kupunguza maambukizi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake

Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Wilaya ya Makete Jonathan Kitundu akizungumza na Kituo hiki,huku akiwasihi wanaume kutahiriwa kwa lengo la kupunguza magonjwa mbalimbali yanayoambukizwa kwa njia ya Kujamiana kufuatia wanaume kutotahiriwa

Daktari Kitundu amesema kwamba baadhi ya Wanawake wanapata Saratani ya Kizazi kwa sababu wanaume wanaoshirikiana nao tendo la ndoa wengine wanakuwa hawajatahiriwa

Ameongeza kwamba wanawake ambao hawajawahi kuzaa mtoto wakipata Saratani za Shingo ya Kizazi hawawezi kupata Watoto waondokane na dhana hiyo kwani inawezekana kupata mtoto/watoto iwapo Mwanamke atawahi kupata Matibabu mapema katika Kituo cha Afya au Hospitali
"Pia niwapongeze Wananchi wa Makete kwa kujitoa kwa wingi kuja hapa Hospitali kupata huduma za Afya na kujua hali zao kwa kupima Saratani ya shingo ya Kizazi"Aliongeza Daktari Kitundu
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG