Serikali
ya Tanzania imeahidi kuanza kuboresha maslahi ya watumishi ya walimu
ikiwemo mishahara yao kipindi hiki kutokana na kumaliza zoezi la muda
mfupi la uhakiki wa wafanyakazi hewa katika sehemu mbalimbali za ajira.
Hayo
yamewekwa wazi na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Joseph
kakunda leo (Jumatano) katika mkutano wa 10 kikao cha saba cha Bunge
kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza
kutoka kwa Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa alipotaka kujua ni lini
serikali itawapandishia mishahara walimu.
"Utaratibu
huu ambao ulikuwa umesimama kwa kipindi kifupi cha miaka kama miwili
hivi kupisha uhakiki wa watumishi ambapo ni zoezi lililofanywa kwa
umahiri na ueledi mkubwa, baada ya kuwa tumelikamilisha sasa tutaingia
kwenye awamu ambayo ni ya kuboresha maslahi ya watumishi ikiwemo
mishahara yao", amesema Kakunda.
Kwa
upande mwingine, Mhe. kakunda amewatoa hofu walimu wote ambao
hawakupandishwa madaraja yao kutokea mwaka 2016 hadi 2017 na kudai
katika mwaka huu wa fedha wameshafanya matayarisho wa kupandisha
madaraja hayo.
0 comments:
Post a Comment