Wahamiaji
83 raia wa Ethiopia na Mtanzania mmoja mkazi wa Tukuyu wamefikishwa
Mahakama ya Mkoa Iringa huku wahamiaji hao wakituhumiwa kuingia nchini
bila kibali.
Akisoma
mashtaka hayo leo Februari 26, 2018, wakili wa Serikali, Godfrey Ngwijo
amesema raia hao wanakabiliwa na shtaka la kuingia nchini kinyume na
kifungu cha sheria namba 45(i) kifungu (1) ,(2) kilichofanyiwa
marekebisho 2016.
Ngwijo
amesema Februari 23, 2018 saa moja jioni katika kijiji cha Mazombe
wilayani Kilolo, wahamiaji 83 wasio na vibali walikamatwa na kufikishwa
kituo cha polisi kwa kuingia nchini kinyume na sheria ambapo dereva wa
lori walilopanda hakupatikana baada ya kukimbia.
Amesema
wahamiaji hao walikamatwa wakiwa katika hali mbaya kutokana na kukaa
sehemu ya nyuma ya lori hilo ambako hakuna hewa ya kutosha, joto kali na
kutokula chakula kwa muda mrefu.
Baadhi ya wahamiaji hao leo wamefikishwa hospitali ya mkoa kupata matibabu.
Wakili
huyo amesema kati ya waliofika mahakamani kusomewa mashtaka yao,
watatu walishindwa kufika kwa sababu bado wako hospitali wanaendelea na
matibabu.
Mtanzania
aliyekutwa katika gari hiyo, Hassan Mwalusanjo akituhumiwa kusafirisha
wahamiaji hao kwa kutumia lori mali ya Gabriel Mwakyambiki mkazi wa
Tukuyu kinyume na sheria, alikana kosa hilo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, David Ngonyani ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 2, 2018.
0 comments:
Post a Comment