Wabunge
na mawaziri kutoka CCM wamejitokeza katika mkutano wa hadhara wa
kampeni kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.
Waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jana Februari 11,2018 katika mtaa wa Idrisa, Magomeni ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako; na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile.
Wabunge
waliohudhuria ni Hussein Bashe wa Nzega Mjini, Azzan Zungu (Ilala),
Livingstone Lusinde 'Kibajaji’ (Mtera), Halima Bulembo (Viti Maalumu) na
Oliver Semuguruka (Viti Maalumu).
Wengine
ni Sixtus Mapumba (Mbinga Mjini), Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu'
(Korogwe), Joseph Musukuma (Geita Vijijini) na Rita Kabati (Viti
Maalumu).
Kabla
ya viongozi hao kupanda jukwaani, burudani ilitolewa na vikundi vya
ushereheshaji huku waliohudhuria mkutano huo wakisimama kucheza na
kuwatuza waliokuwa wakiburudisha.
Halima
lisema mwanzoni Mtulia alikuwa mbunge wa upinzani na katika baraza la
madiwani hakuweza kushauriana na meya lakini sasa yuko CCM hivyo
kuwaomba wananchi wamchague.
Mapunda alisema wananchi wa Kinondoni hawakuwa na tatizo na mchezaji bali timu anayochezea.
“Mchezaji
mzuri akitoa pasi inaharibika na ndiyo maana Mtulia ni mchezaji mzuri
na sasa amekuja timu bora ya CCM mleteni tumalize mchezo mapema,”
alisema.
Mbunge Zungu alisema wabunge wa CCM hawana ujanja bali ni ilani ambayo imejenga kuwajali wananchi.
Dk
Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni alisema, “Mtulia nitampa
ushirikiano katika kutatua matatizo ya afya, wazee na maendeleo ya jamii
yatapatiwa ufumbuzi kwa kumchagua Mtulia.”
0 comments:
Post a Comment