Rais
waJamhuriya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
ametekeleza ahadi yake ya kumsaidia Bajaj Mlemavu wa viungo Bw. Yusuf
Abdulrahaman Ndemanga.
Bw. Ndemanga amekabidhiwa Bajaji hiyo na Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 02 Februari, 2018.
Mhe.
Rais Magufuli alikutanana Bw.Ndemanga tarehe 25 Agosti, 2017 katika
sehemu ya abiria wakati akisubiri kupanda kivuko cha MV Magogoni
kuelekea Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kukutana na Mhe. Rais Magufuli, Bw. Ndemanga alimuomba msaada wakupatiwa Bajaj iliimsadie kupata kipato.
Akikabidhi
msaada huo Bw. Ngusa Samike amemtaka Bw. Ndemanga kuitumia Bajaj hiyo
vizuri nakujiongezea kipato kitakacho msaidia yeye na familia yake.
“Mhe.
Rais amenituma nikukabidhi Bajaj hii mpya kabisa, matarajio yake nikuwa
itakusaidia kupiga hatua za kimaendeleo, anatarajia kukuona unaongeza
Bajaj nyingine na unaisaidia familia yako kupata nafuu ya maisha na sio
kuja kuomba msaada mwingine” amesema Bw. NgusaSamike.
Kwa
upande wake Bw. Ndemanga aliyeongozana na Mkewe Bi. Hawa Mohamed
amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa msaada huo na ameahidi kuwa ataitumia
Bajaj hiyo vizuri kuzalisha kipato kwa ajili ya familia yake.
0 comments:
Post a Comment