Mwanamuziki Bongo Fleva, Shilole amedai
kuwa hana ujauzito wa mumuwe Uchebe kama watu wanavyomdhania baada ya
kumuona amenenepa sana hivi karibuni.
Shilole amedai kuwa mume aliyenaye anamfanya anenepe. “Sina Ujauzito,
ila watu wananiombea mema, mume niliyenaye ananifanya ninenepe”.Akongeza kuwa dada yake alimkataza yeye kuolewa na Uchebe. “Dada alimkataa Uchebe kwa sababu anaonekana hana kipato kikubwa.”
Kwa mujibu wa wapenzi hao wamedai kuwa walikutana kisiwani Zanzibar na huki ndiko mapenzi yao yalipoanzia baada ya Uchebe ambaye ni mumuwe kuamua kueleza hisia zake.
0 comments:
Post a Comment