Watangazaji
wa Kipindi maarufu cha Shilawadu kinachorushwa na Clouds tv,Soudy Brown
na Kwisa wamechezea kichapo kutoka kwa Dancer wa Diamond,Mose
Iyobo,usiku wa kuamkia ijumaa,baada ya kutaka kumuhoji kuhusu matukio
yaliyotokea hivi karibuni kati ya familia yake na mwanadada Tunda.
Wakithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Shilawadu wameandika katika ukurasa wao wa instagram:
Kazi yetu ina changamoto kubwa sana..asilimia kubwa ya ma star wanatuunga mkono.
Usiku
wa Leo wakati tukiwa kazini tumenusurika kumwagwa damu na mtu
tuliemfuata kumuomba kufanya naye mahojiano,kati yetu kuna walioumia
viuno,mikono, etc.kuna uharibifu wa vifaa vyetu vya kazi umetokea
pia,wenzetu wanaendelea na matibau Mungu ni mwema Mungu ni wetu sote
na hili litapita bado tuna wasiwasi tu kama mhusika ataendelea
kututafuta kwa ajili ya kutudhuru zaidi,tunasikitishwa sana na matumizi
ya nguvu dhidi yetu sisi Wanyonge #Shilawadu
Kuna
watu watasema Shilawadu wamezidina kusahau kuwa sisi ni wana Habari
kama wanahabari wengine na kupata habari ni haki ya kila mwananchi kama
ilivyo haki nyingine yoyote ile.Kifungu cha 18 cha katiba ya Jamhuri ya
Muungano 1977 na hatimaye kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 inampa haki
mtu na uhuru wa kujieleza na kutoa mawazo,uhuru wa kutafuta
habari,kupata habari,na kuneza habari bila kujali mipaka,pia sheria hiyo
inampa haki mtu ya kuwasiliana bila kubughudhiwa na mawasiliano na
kufahamishwa wakati wowote masuala yoyote muhimu yahusuyo maendeleo yake
na yahusuyo jamii yake kwa ujumla.
Imeandikwa na Mtayarishaji wa Kipindi cha Shilawadu Benedict Noel
0 comments:
Post a Comment