Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon
Sirro ameitaka jamii pamoja viongozi wa dini kushirikiana na Polisi ili
kutokomeza makosa mbalimbali katika jamii ikiwemo mauaji yatokanayo na
wivu wa mapenzi, ulevi, ubakaji ili kuiweka nchi salama zaidi.
IGP Sirro ameeleza hayo leo Jijini Dar es
Salaam ambapo amesema kuwa takwimu za sasa zinaonyesha matukio ya aina
hiyo yamekithiri sana nchini Tanzania jambo ambalo jamii inapaswa
kubadilika ili kupunguza matukio hayo.
“Kuna makosa ambayo watu lazima
wabadilike na hili haliitaji Jeshi la Polisi maana mimi nasimamia
Sheria lakini kuna viongozi wa dini wazungumzie hayo mambo. Muumini
wako akija Kanisani au Msikiti na ukimwambia katazo la Mungu anaweza
akabadilika”,.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini IGP Sirro amesema kuna makosa ambayo viongozi wa dini
wakishiriki kwa ukaribu zaidi inaweza kupunguza huku akiitaka jamii
kubadilika kitabia ikiwemo kuachana na ulevi wa kupindukia.
0 comments:
Post a Comment