Rais
wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametuma
salamu za pole kwa familia ya Akwilina Akwilini aliyeuawa baada ya
kupigwa na risasi katika maandamano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Februari 16, 2017 eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam
Katika
salamu hizo, Rais Dkt Magufuli amesema kwamba amepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa za kifo hicho na hivyo ameviagiza vyombo vya dola
kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote
watakaobainika kuhusika na tukio hilo.
“Nimesikitishwa
sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji
(NIT). Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa
na msiba huu. Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na
kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili.”
Akwilina
alikumbwa na umauti wakati Polisi walipokuwa wakitawanya maandamano ya
CHADEMA walipotaka kwenda kwenye Ofisi za Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo
la Kinondoni kuhoji kwanini mawakala wao hawajaaapishwa.
0 comments:
Post a Comment