Aliyekuwa
Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji amefunguka na kuweka wazi
msimamo wake juu ya tukio la kupigwa risasi kwa mwanafunzi wa mwaka wa
kwanza Chuo cha NIT Aqulina Akwilini na kusema kuwa chama chake cha CCM
hakiwezi kukwepa juu hilo.
Shy-Rose
Bhanji amesema kuwa kufuatia kifo hicho cha mwanafunzi huyo ambaye
alipigwa risasi na jeshi la polisi Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni
jijini Dar es Salaam wakati jeshi la polisi likiwatawanya wafuasi wa
CHADEMA ambao walikuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa
Kinondoni na kudai kuwa suala hilo yeye linamsuta moyoni mwake.
"Serikali
ya chama changu CCM haiwezi kukwepa lawama kwa namna yoyote ile
kufuatia kupigwa risasi kwa binti ambaye hakuwa na hatia hata kidogo.
Imekuwa ni siku mbaya sana kwangu, nimeshindwa kula na nashindwa kupata
usingizi kutokana na kifo cha huyu binti. Nafsi yangu inanisuta. Mungu
wangu naomba unisaidie" alisema Shy-Rose Bhanji
0 comments:
Post a Comment