Polisi
inawashikilia askari wake sita na silaha zao kwa ajili ya uchunguzi
kuhusu tukio la kuuawa kwa risasi mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT), Akwilina Akweline.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hayo
leo Februari 18,2018 alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ulinzi
wakati wa kampeni, upigaji kura, na utangazaji matokeo ya uchaguzi
mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni uliofanyika jana Februari 17,2018.
Amesema
polisi iliunda timu ya upelelezi kuchunguza chanzo cha kifo cha
mwanafunzi huyo kilichotokea Februari 16,2018 wakati polisi
wakiwatawanya wanachama wa Chadema waliokuwa wanakwenda ofisi za
mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kushinikiza mawakala wao kupatiwa
barua za viapo vyao.
Kamanda
Mambosasa amesema polisi pia inawachunguza watuhumiwa 40 ili kubaini
iwapo miongoni mwao walikuwepo waliokuwa na silaha za moto.
Amesema
pia wanaendelea kuwatafuta wafuasi na viongozi wa Chadema walioshiriki
kushawishi wafuasi wao kushiriki kwenye maandamano.
Wakati
huohuo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole katika
taarifa aliyoitoa jana Februari 17,2018 alisema chama hicho kinalitaka
Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu aliyehusika na tukio la
kuuawa kwa mwanafunzi huyo.
Polepole
alisema polisi imhoji Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi
wenzake walioshiriki maandamano aliyosema hayakuwa halali
yaliyosababisha uhai wa Mtanzania kupotea.
0 comments:
Post a Comment