Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
amemtembelea muigizaji mkongwe, Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini
jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa.
Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara.
“Mimi
ndiyo mtu wa kwanza kumtabiri kwamba akiwa Rais itakuwa shughuli.
Nilishukuru sana kuchaguliwa huyu bwana, tumepata Rais sio masihara watu
wote sasa hivi wana adabu zao wanajua nini maana ya kazi”, alisema Majuto.
Pamoja na hayo, Mzee Majuto aliendelea kwa kusema ;“sisi
wazee tunafarijika sasa hivi, viwanda kila kona vimetapakaa na leo
amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko
kwa uoga maana hataki masihara. Hii ndio raha ya kupata viongozi wenye
msimamo”.
Kwa
upande mwingine, Mzee Majuto amesema sio rahisi kupata Rais mwenye
misimamo na asiyekuwa na masihara kama Dkt. John Magufuli.
0 comments:
Post a Comment