Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako pamoja na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Injinia Hamad Masauni wakimfariji Mama
Mzazi wa marehemu Aqwilina jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar.
***
Mwanafunzi
huyo wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya
kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es
Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya chama cha
CHADEMA.Kufuatia kifo cha Mwanafunzi huyo Serikali imesema itabeba
jukumu la Mazishi yake.
Aidha
Rais Dkt John Pombe Magufuli amesema amesikitishwa sana na kifo cha
mwanafunzi huyo,Aqwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT).
"Natoa
pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba
huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua
za kisheria waliosababisha tukio hili",Ilisema sehemu ya taarifa yake iliyotolewa mapema leo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako (tatu
kulia) akiwafariji Mama Mzazi wa marehemu Aqwilina pamoja na ndugu
jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar
Mama
wa Marehemu Akwiline akilia kwa uchungu mara baada ya kuona viongozi wa
Waandamizi wa serikali walipofika nyumbani kwake,Mbezi Kimara jioni ya
leo kwa lengo la kutoa pole na kufahamu taratibu mbalimbali za msiba
huo.
0 comments:
Post a Comment