Kutokana
na umuhimu wa mwanafunzi kupata chakula shuleni, wakati mwingine
huwalazimu walimu kutoa gharama zao wenyewe kuwanunulia chakula
wanafunzi ambao wazazi wao hawajachanga fedha ya chakula
Hayo
yamesemwa na Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ikonda Enerika Kayombo na
kusema yeye ni mmojawapo wa mwalimu ambaye amekuwa akitoa gharama zake
kuhakikisha wanafunzi ambao hawajachangiwa chakula na wazazi wanapata
chakula
"wakati
wenzao waliochanga wanakula chakula, ambao hawajachanga unakuta
wanakuwepo eneo wanapopata chakula wenzao, unawafukuza lakini wakati
mwingine inakulazimu kugharamia ili wale, binafsi nimefanya hivyo,
kamati ya shule ni mashahidi" amesema mwalimu huyo
0 comments:
Post a Comment