Raia kadhaa wa Syria wanatibiwa baada ya kushindwa
kupumua kutokana na mashambulizi ya ndege yaliyofanywa na serikali
kwenye mji wa Saraqeb.
Shirika linalofuatilia haki za binaadamu nchini Syria lenye makao
yake mjini London, Uingereza limesema raia watano wanapatiwa matibabu
kutokana na kukosa pumzi na kushindwa kupumua baada ya serikali ya Syria
kutumia silaha za sumu katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi kwenye
mji wa Saraqeb uliopo kaskazini magharibi mwa Syria.
Duru za
kitabibu zimeeleza kuwa wagonjwa wengine 11 walikuwa wakitibiwa kutokana
na gesi yenye sumu ya Chlorine, iliyotumika katika shambulizi hilo.
Shambulizi hilo limefanyika siku chache baada ya Marekani kuishutumu
serikali ya Syria kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya vikosi vya
waasi karibu na mji mkuu, Damascus.
Hata hivyo serikali ya Syria
imekanusha madai hayo ikiyaita kuwa ni ''uongo''. Siku ya Ijumaa Waziri
wa Ulinzi wa Marekani, Jim Mattis aliwaambia waandishi habari kwamba
serikali yake ina wasiwasi gesi ya sarin huenda ikawa imetumika hivi
karibuni nchini Syria, ikizinukuu taarifa za mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali pamoja na makundi ya waasi.
0 comments:
Post a Comment