Maofisa
watatu wa Jumuiya ya Ulaya (EU) jana Februari 5,2018 wamemtembelea
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayeendelea na
matibabu nchini Ubelgiji.
Lissu
alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30, Septemba 7 mwaka jana na
kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa
Hospitali ya Nairobi alilazwa hadi Januari 6,2018 alipohamishiwa
Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na
matibabu.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana Februari 5,2018 Lissu
amewataja maofisa hao kuwa ni Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na
Afrika Mashariki katika Wizara ya Nje ya EU, Patrick Simonnet.
Wengine
ni Mkuu wa Dawati la Tanzania katika EU, Marta Szilagyi, Vania
Bonalbert ambaye ni ofisa wa ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia
masuala ya utawala bora na haki za binadamu na Hortensia May Lyatuu.
Amesema ujumbe wa maofisa hao mbali ya kumjulia hali walifanya mazungumzo ya masuala mbali mbali yanayohusu Tanzania.
0 comments:
Post a Comment