Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amesema Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko ya dhati katika sekta ya
utalii kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa barabara na pia kuweka
mikakati dhabiti ya kuviendeleza vivutio vya utalii viliovyoko kanda ya
Kusini ili vichangie ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.
Makamu
wa Rais aliyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa
kuendeleza utalii kanda ya kusini mwa Tanzania uliofanyika Kihesa Kilolo
mkoani Iringa.
Makamu
wa Rais alisema Serikali imeendelea kuandaa na kutekeleza mipango
mikakati mabali mbali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za utalii
zinasambaa nchi nzima .
Makamu
wa Rais amasema katika kuendeleza utalii kanda ya kusini, ambapo
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo mwenye
masharti nafuu Dola za kimarekani milioni 150 kutoka benki ya Dunia
ambapo mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6 kuanzia 2017/2018.
Mradi
huo wenye lengo kuu la kukuza utalii na kipato kwa wananchi kwa
kuboresha miundo mbinu, kujenga uwezo katika usimamizi wa maliasili na
kuwawezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija
“Kama
nilivyosema hapo awali mradi huu utajulikana kama Resilient Natural
Resource for Tourism and Growth (REGROW) na utaanza kutekelezwa katika
maeneo ya hifadhi ya Taifa za Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba
Selous “
Makamu
wa Rais ameiagiza Baraza la Mazingira lililokuwa chini ya Ofisi yake
kuharakisha tathmini ya mazingira ya bonde la mto ruaha mkuu ili
kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi bila athari zozote
baadaye za mazingira.
Makamu
wa Rais alielekeza taasisi zote zinazohusika zikiwemo Sekretarieti za
mikoa, Halmashauri za Wilaya na Vijiji kutoa ushirikiano wa kutosha wa
kufanikisha utekelezaji wa shughuli za mradi.
“Tuhakikishe
sheria zinafuatwa na hakuna uvamizi wala shughuli za binadamu kwenye
vyanzo vya maji na hifadhi. Wahenga wanasema tunza mazingira yako
yakutunze”.
Makamu wa Rais aliwashukuru benki ya Dunia kwa kukubali kukopesha mkopo wenye masharti nafuu .
Aidha
kabla ya Makamu wa Rais kuzungumza, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.
Dkt. Hamisi Kigwangalla alisema Sekta ya Utalii ni moja ya sekta za
kipaumbele katika uchumi wa Tanzania ambapo takribani asilia 20 ya pato
la Taifa linatokana na utalii na robo ya fedha za kigeni zinatokana na
Utalii.
0 comments:
Post a Comment