Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amemwagiza Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi
wa Maji Mijini, Clement Kivegalo.
Pia,
Kamwelwe amemwagiza mkurugenzi wa utawala wa wizara hiyo, Barnabas
Ndunguru kuwahamishia Dodoma watumishi 178 wa wizara ifikapo Januari
30, 2018 la sivyo atamchukulia hatua.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Januari 20, 2018 jijini Dar es Salaam,
Waziri Kamwelwe amesema jana Januari 19, alizivunja bodi za maji safi
za Mkoa wa Arusha na Musoma baada ya kujiridhisha kuwa utendaji wao si
mzuri.
“Juzi
tu niliuondoa utendaji wa Lindi, kuna tatizo la utendaji wa wakandarasi
hapa Dar es Salaam, Chalinze na tuna tatizo Kigoma, mamlaka za maji za
miji ya mikoa zinasimamiwa na mkurugenzi wa maji mijini, hapa tuna
idara kama tatu au nne zinasimamia utekelezaji wa miradi hiyo,” amesema
Mhandisi Kamwelwe na kuongeza,
“Idara
ya maji mijini inaongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mhandisi Clement Kivegalo
wakati haya yote yanatokea Kivegalo yupo lakini matatizo yanatokea
yanabainiwa na waziri, naibu waziri au katibu mkuu, leo Januari 20, 2018
namwagiza Katibu Mkuu atengue uteuzi wake atafute mtu mwingine.”
Waziri
Kamwelwe amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyeko ziara mkoa wa Mara
amebaini kasoro za utendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Musoma (Muwasa) na kuagiza hatua zichukuliwe ikiwamo
kuchunguzwa watendaji wote.
“Kupitia
ziara ya Waziri Mkuu imebainika yapo matatizo yanayomhusu mkurugenzi wa
Muwasa, Gantara Said na wahusika wote ameeleza wafanyiwe uchunguzi,
hivyo kuanza leo Januari 20, natengua uteuzi wake na nafasi yake
itakaimiwa na Petro Muhoja wa Mamalaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira
Mwanza, namwagiza mkurugenzi wa mamalaka ya maji Mwanza, asaidie
mamlaka ya maji Musoma ili waweze kufanya kazi,” amesema.
0 comments:
Post a Comment